Mtelezo-theluji na kupanda kwenye miamba huweza kukuweka hatarini na wengine huathiriwa na miji na majiji.Kwa mfano mji wa Leadvile Colorado iko juu ya m.3000.Milima mikuu katika Amerika ya kaskazini iko katika Latitudo za Kaskazini,ambapo kanihewa ni ya chini kiukanda wa juu kuliko kwenye Ikweta.
Katika milima ya Andesi ni rahisi kupaa au kuendesha katika maeneo kama Cusco(m.3,326) au La Paz(m.3,600) bila kujizoeza mazingira ya njiani.Ni vema upumzike kwa muda kisha uachane na mambo mengi kwa siku kadhaa kabla hujajaribu safari za nyanda za juu kama Inca trail.
FIFA imezuia mechi ya mashindano ya kimataifa ya mpira wa mguu huko La Paz, Bolivia kwani timu ya nyumbani ina nafasi kubwa ya kushinda kwani wamezoea mazingira asilia ya ukosefu wa Oksijeni.
Mfanyabiashara aliyetarajia kupata mkataba wa mamilioni ya madola aliruka kwa ndege huko La paz(m.3600) Bolivia siku moja kabla ya mkutano adhimu sana.Kampuni yake iliamua kuweka akiba kwa ajili ya kumpeleka siku chache mapema ili aweze kuzoea mazingira.Aliugua mno na hata alipokuwa anawasilisha hoja akapoteza ushawishi wa kukidhi haja ya mkataba.Wakati mwingine ujao atahakikisha anapata muda wa maandalizi.