The Main Signs
Dalili kuu:
• Kushindwa kupumua.
• Uchovu na uchakavu.
• Kikohozi.
• Makohozi yenye mapovu na baadaye damu kwenye makohozi atemapo.
• Midomo, ulimi na makucha hugeuka kuwa bluu.
HAPE inaweza kuonekana kati ya saa 1-2 au siku nyingine na hata wakati wa kushuka.
Can they?
Kagua haya:
• Kumekuwepo upandaji kwenye nyanda za juu karibuni?
• Je, muda mrefu hutumika kurejesha pumzi baada ya mazoezi?
• Anapata shida ya kupumua akiwa amepumzika?
• Anapumua haraka?
• Je, kifua kinalia mgonjwa apumuapo? Tia masikio nyuma chini ya viriba vya mabega
What to do
Cha kufanya:
• Kaa na mgonjwa kipindi chote, asiachwe mwenyewe.
• Shuka haraka sasa hivi – si baadaye au kesho yake.
• Wakalishe wima na wape joto.
• Wape oksijeni kwenye mtungi au mfuko wa shinikizo kama unayo.
• Mpe nifedipine ukiwa nayo.
• Mpe acetazolamide ukiwa nayo.
• Kama hajiwezi kabisa na hawezi kushuka, mfuko wa shinikizo litahitajika kutumika kwa muda mrefu.
Consequences
Madhara ya kutojali:
Kuacha kupumua.
KIFO.
Kwenye kesi mbaya, kifo kinaweza kutokea kwenye lisaa limoja baada ya dalili kuonekana.
Kumbuka: unaweza kupata AMS, HACE na HAPE wakati huohuo.
SHUKA HARAKA SHUKA HARAKA SHUKA HARAKA