Ukiwa una kampuni ya utalii na unawaajiri wachukuzi kukusaidia kubeba mizigo unawajibika kwao.Ni lazima uzilinde afya na usalama wao-ni muhimu kama afya yako binafsi.
Wachukuzi wenye kazi ya uchukuzi wa mizigo.Huweza kuathirika na magonjwa ya milimani kama mgeni apatavyo.Huko nyuma wachukizi walipougua walionekana hovyo, wakalipwa na kuachwa wenyewe washuke.Wengi walipoteza maisha njiani.
Shirika la kimataifa la kuwahami wachukuzi (IPPG) wameweka utaratibu maalum ambao kila upande kwenye mkataba lazima wauzingatie.Ikiwa ni pamoja na:
– Mastakimu
– Chakula na vinywaji vya kutosha
– Matibabu na bima ya afya ya maisha
– Uangalizi wakati wa kushuka endapo yote yatashindikana
– Mzigo unaohimilika.
Maswali ya kuuliza makampuni (au ya kujiuliza)
1. Je, kampuni unayotaka kuingia nayo mkataba huzingatia muongozo wa kimataifa wa usalama kwa wachukuzi maarufu kama IPPG?
2. Ni nini sera yao ya zana na afya kwa wachukuzi?
3. Hufanya nini kuhakikisha kwamba rasilimali watu wa safari zao hupata mafunzo ya haja kuwatunza wachukuzi wao?
4. Ni nini sera yao ya mafunzo na usimamizi wa huduma bora kwa wachukuzi kwa wenye kampuni ya kitalii?
5. Je, kuna kipengele kwenye dodoso lao la mrejesho kwa wateja wao katika safari zilizopita zinazohusu huduma kwa wachukuzi?
Kulbahadur, mchukuzi mwenye umri wa miaka 33 aliachwa na kikundi chake alipokuwa mgonjwa mno hata asiweze kubeba mizigo kwenye hifadhi ya taifa ya mlima Everest.Baadaye akaokotwa na kundi lingine la watalii taratibu akiendelea kupoteza miguu yake kwa baridi ya barafu.Hakujua jina la kampuni wala uraia wa watu aliyokuwa anawatolea huduma.