Watu huenda nyanda za juu kwa hali zao za awali za kimatibabu.Ukiwa miongoni, ongea na daktari upate ushauri endapo ni vema kukwea mlima ama la.Na kama ukienda ni kwa vipi ujilinde.
Kwa hali yoyote kuna hatari zaidi kiafya usafiripo safari za masafa.La msingi ni kupunguza hatari iwezekanavyo.Jiandae kujinyima kwa ajili ya sababu za kiusalama safarini.
Kwenye uwanda wa juu:
• Tafadhali ambatana popote ulipo na taarifa za tiba/ bangili la tahadhari ya tiba.
• Kila siku tia kwenye shajara kila taarifa zako za matumizi ya dawa na mabadiliko yatokeayo mwilini mwako.
• Dalili zikiongezeka ukiwa unapanda juu, usiendelee kupanda. Fikiria uwezekano wa magonjwa yanayohusiana na nyanda za juu, shuka haraka iwezekanavyo.
• Eleza ukweli wa hali yako ya kiafya kwa kila unayeabiri naye.
• Walinde wanafamilia, marafiki na wasafiri wengine.
Maandalizi:
• Muone daktari/daktari wako bingwa miezi sita kabla ya ziara. Uchunguzwe hali zinazoweza kuhatarisha maisha yako kwenye uwanda wa juu.
• Uwe na mpango wa tiba na kama kuna usaidizi utakaouhitaji. Chunguza usaidizi wa kimatibabu utakaopatikana. Tafakari kuhusu mbadala wako endapo litatokea.
• Andika mawasiliano ya sehemu uendako.
• Hakikisha kila mtu anaelewa hali yako ya kiafya, viashiria, dalili na tiba. Ugonjwa wako unaweza kuwaathiri wanakikundi wote wakati wa ziara.
• Jipatie elimu ya huduma ya kwanza kwa ajili yako na wengine.
• Fungasha dawa maelekezo yawe wazi. Uwe na ziada ya upatikanaji wake, wape watu wengine baadhi ya dawa kuepuka upotevu wake wote.
• Muombe daktari akuandalie barua ya kiofisi ielezayo hali yako ya kiafya, matibabu na kuwasiliana nao kwa lolote linaloweza kutokea.
• Mueleze muuguzi wako kuhusu hali yako kabla ya kupata chanjo n.k.
• Uwe na bima ya afya itakayolinda hali yako ya kiafya wakati wa ziara. Huweza kuwa ngumu na ghali au kutowezekana kwa baadhi ya mahitaji ya wasafiri wengine.