Site Loader

Afrika

Tatizo kuu hutokea mlima Kilimanjaro,ambapo gharama huzingatia idadi ya siku unazotumia mlimani.Wageni wengi hulazimika kupanda haraka kuliko inavyotakiwa-m.300 kwa siku.Inawezekana kutumia muda kwenye vijilele vya jirani kujiandaa kabla ya kilele chenyewe.

Makampuni mengine ya kitalii yameanzisha taratibu zinazozingatia hili.Ni bora kutumia ziada kidogo ili uwe salama na kufikia malengo yako.Wasiliana na makampuni safari za mbali ili zikueleze ni watalii wangapi hawakuweza  kufika kileleni (Uhuru au Gilman)katika safari za hivi karibuni.Waulize idadi ya siku walizotumia.Safari salama ni vema ikatumia siku 8 hadi 10.

Mwingereza mwongoza watalii mzoefu na mwenye elimu ya tiba za mlimani alikuwa akiwaongoza kundi la watalii kulekea kilele cha mlima Kilimanjaro(m.5895).Wakakutana na kundi lililojaa hofu na lenye kijana mmoja mwenye miaka 17 aliyezimia njiani akipanda.Mwongoza watalii akamdunga sindano ya pumu(dexamethasone) wakati huohuo akiharakisha kumshusha chini kuokoa maisha yake.Alipofika kwenye kibanda cha kupumzikia,alitumia simu yake ya Setilaiti kuwasiliana na tabibu mwingereza mkwezi aliyeshauri washuke zaidi usiku.Siku mbili baadaye,kijana alikuwa mzima na uzima wake.Endapo angelikuwepo mwenye ueledi wa magonjwa ya nyanda za juu,dharura ingeepukwa.Chakusikitika walijifunza somo hili katika njia ngumu na isiyoepuka.

Previous         Next