The Main Signs
Dalili Kuu:
• Kuumwa kichwa sana.
• Ugoigoi.
• Kuwa na tabia za ajabu: kutosaidia, mwenye hasira, mvivu.
• Unaweza kukabiliwa na matapishi yasioisha.
• Uoni halifu.
• Unaweza kuona, kusikia, kupata harufu ya vitu vya ajabu.
• Unaweza kuchanganyikiwa.
• Upungufu wa fahamu.
Can they?
Chunguza haya:
• Kugusa pua kwa kidole cha shahada? Rudia haraka
• Kutembea kwa kugusa kisigino na vidole vya mguuni katika mstari mnyoofu?
• Kusimama wima huku umekunja mikono na kufumba macho?
• Kufanya kesabu rahisi za kichwa?
Kama huwezi kuyafanya yote hapo juu au kupata shughuli kuyafanya, jishuku kwa HACE
HACE huweza kutokea haraka sana bila shida yeyote nyingine au baada ya AMS na HAPE.
What to do
Cha kufanya:
• Kaa na mgonjwa kipindi chote – usimwache mwenyewe.
• Shuka muda huohuo- sio baadaye au asubuhi yake.
• Wakalishe wima na wape joto.
• Wape oksijeni kwenye mtungi au mfuko wa shinikizo kama unayo.
• Wape dexamethasone ukiwa nayo.
• Wape acetazolomide ukiwa nayo.
• Kama hajiwezi kabisa na hawezi kushuka, mfuko wa shinikizo litahitajika kutumika kwa muda mrefu
Consequences
Madhara yanayoweza kutokea kama hatua hazitachukuliwa:
Kupoteza fahamu – kuchanganyikiwa, usingizi mzito.
Kuhema kwa shida.
KIFO.
Kwenye kesi mbaya, kifo kinaweza kutokea kwenye lisaa limoja baada ya dalili kuonekana.
Kumbuka: unaweza kupata AMS, HACE na HAPE wakati huohuo.
SHUKA HARAKA SHUKA HARAKA SHUKA HARAKA