Kwa sababu kuna upungufu wa hewa ya oksijeni kwenye nyanda za juu, kuvuta hewa huwa kwa haraka na kina ili kufidia. Hii aklimataizesheni- kutumia oksijeni kidogo kwenye miinuko, hukusaidia kujisawiri vizuri katika mwinuko. Kupungukiwa na pumzi kwa zoezi sawa na hili kwenye mwambao wa pwani ni kawaida.
Kuna mabadiliko mengine yanayotokea kwenye damu bila kujua kwa azma ya kuelekeza damu ya kutosha inakohitajika.
Zaidi, watu hupatwa na kikohozi kikavu kwenye nyanda za juu. Hakuna ajuaye kwa hakika ni kwa nini hilo hutokea, ingawa huchochea tishio.
Mara nyingine matatizo mabaya ya kupumua hutokea.
Kunaweza kutokea mafundo ya maji kwenye mapafu na kusababisha maji kwenye mapafu, maarufu kama HAPE. Dalili zikiwa pamoja na kushindwa kupumua wakati umepumzika na hata makohozi ya damu iliyoganda huonekana. Watu ambao wamewahi kuugua ugonjwa huu wanaweza kuupata tena, mara nyingi katika mwinuko sawa. Hili ni tatizo kubwa na haipaswi kutojali.
Kwenye uwanda wa juu:
• Tembea taratibu.
• Pumzika vya kutosha.
• Sio ushindani! Wengine huzoea mazingira haraka.
• Usithubutu kutojali dalili za HAPE! Ikiwezekana pata ushauri wa daktari na kama unasita SHUKA CHINI
Maandalizi:
• Fanya mazoezi kila mara hasa ya nyanda za juu; usipungukiwe pumzi kwa kukosa ustahimilivu!
Mpandaji milima mzoefu katika safari ya utafiti wa matibabu alifika katika m.5200 akajikuta damu imepoteza kiwango cha oksijeni ambacho kingemuwezesha kuishi.Mapafu yake yaliendelea kujaa maji, alishikwa na kizunguzungu na kushindwa kupumua usiku.Kushuka hakukuwezekana pasi na kupitia njia nyembamba za juu za milimani.Alipewa vidonge vya acetazolamide mg.500 kisha mg.250 mara tatu kwa siku. Baada ya saa 24 na kukojoa kwake kwingi, kiwango cha oksijeni kilipanda hadi kufikia kinachotakiwa.