Wengine hali zao huzorota zaidi jinsi baridi na mazoezi zinavyoendelea kushambulia. Wengine hupona jinsi miili yenyewe inavyojiongezea steroidi na kupunguza mizio ya hali ya hewa.
Kwenye uwanda:
Uwe na vifaa vyako vya pumzi kokote uliko.
Punguza matatizo kwa kupunguza shughuli, tumia dawa unapolazimika kufanya hivo na shuka kama hujisikii vizuri.
Epuka dawa chochezi kama aspirini na ibuprofeni.
Maandalizi:
Usiondoke hadi pumu iwe imetulia.
Hakikisha umepata chanjo za kisasa nay a mafua.
Hakikisha umebeba vipumzishi na stiroidi za kutosha.
Elewa visababishi vya pumu lako na viepuke.
Fanya majaribio, anza na nyanda za chini na viwango vya chini vya uchovu.