Ubongo huathiriwa na nyanda za juu kwani huhitaji oksijeni ya kutosha na huweza kuvimba na kusababisha mkazo.
HACE husababishwa na uvimbe ubongoni na huweza kuua ghafla kama haiwahi kutibiwa.Wengine hawahisi madhara yoyote,hata hivyo huweza kuugua yote haya:
Kuumwa kichwa; ni kawaida mwinukoni,hususan kama huumwa kichwa nyumbani mara kwa mara.
Kutojimudu/kukosa balansi:Uratibu na kukosa balansi kunaweza kuathiriwa.Watu wazima na wale wanaoweza kutumia oksijeni kidogo huhisi taathira kidogo.
Ugoigoi na maamuzi mabovu huongeza hatari ya ajali.
AMS/HACE– tazama kurasa zingine.
Kiarusi: Kupata magonjwa ya uoni na mazungumzo au kudhoofika kwa mikono,miguu au uso ni dalili za kiarusi(wanaugua kipandauso wana taathira sawa wakati wa ‘aura’)
Kwenye uwanda:
• Kuumwa kichwa (AMS) epuka sababishi- upungufu wa maji mwilini, uchovu, pombe- tibu na dawa za maumivu .
• Kiarusi- tibu na nusu kidonge cha 300mg ya aspirin & shuka chini. Mwone daktari.
• Kuwa mkweli na unavyojisikia.
Kabla hujaondoka:
• Jifunze viashiria vya maji kwenye ubongo na kiarusi
• Andaa dawa
• Fikiria matarajio/hofu na nani atakayekupa msaada wakati wa shida
Niliong’oa nanga nikiwa naumwa kichwa,nikikohoa.Kichwa na kikohozi changu viliendelea kwenda mrama.Nikaanza kuongea kwa kuvuta maongezi.Nilipokutana na wengine nikawauliza kama kuzungumza kwangu kulikuwa kwa kukokoteza maneno.Nilijikia mwenyewe nikimumunya hovyo maneno.Walishtushwa,maneno yaliendelea kunitoka kidogokidogo.Sikuwa na uwezo wa kutumia mkono wangu wa kulia,ulituama na upande wa kushoto usoni ulikuwa kwenye tufani ya kiarusi na kichwa kuuma.Nilisalia mikono mwa wataalam wa afya na huduma za dharura.