Aghalabu haya ndiyo huonekana sana:
- Maumivu ya kichwa
- Kichefuchefu
- Uchovu
- Kukosa hamu ya kula
- Kizunguzungu
- Kutopata usingizi.
Kielelezo rahisi cha alama kimeoneshwa katika ukurasa unaofuata,na kwa waabiri wa Medex kila mmoja hutazama rekodi za alama zao mara mbili Kwa siku.
Ni vizuri kama kila mmoja akayarekodi maendeleo yake asafiripo na aueleze ukweli msafara wake(chukua nakala ya fomu nyuma ya kitabu hiki).Kila mmoja anaweza kuchangia kwenye maamuzi ya busara-kuendelea kupanda na safari,kupumzika au kushuka.Kama kundi,afya ya kila mmoja ni muhimu.
Kuficha ugonjwa au kumlazimisha mtu kuendelea na safari ni hatari.
Baadhi ya watu huonekana wakizoea polepole kutumia oksijeni kidogo na huhitaji mambo taratibu.
Ukiwa dhaifu,haimaanishi kwamba muelekeo wako wa upandaji ni wa hatari,la hasha, bali ukijilazimisha,huweza kuwa hatari.Kama hujazoea kufanya mazoezi ya mwili,kujihisi mchovu safari ni kawaida.Hali kadhalika ulalapo kwenye hema usiku na hujapazoea,kulala kwako kunaweza kusikupendeze.Lishe nayo inaweza kuwa tofauti.
Muhimu sana ni kwamba dalili zinazidi kuwa mbaya au zinapungua.
Kama unadhani afya inazidi kudhoofika, shuka (m.500-1000 kwa ajili ya usingizi). Jipe muda wa kutosha wa mwili kuzoea matumizi ya oksijeni kidogo.
Usiyapuuzi maamuzi haya hadi mambo yakaenda kombo.
Kwenye uwanda wa juu:
• Kama unahisi maumivu ya kichwa na jumla ya 3 au zaidi ya vingine, usiendelee kupanda.
• Kama unaumwa kichwa na jumla ya 3 au zaidi kwa vingine, huko sawa wala vizuri, rudi chini.
Kabla ya kuondoka kuelekea safarini:
• Jifunze dalili za AMS
• Ukitaka kutumia Diamox- jifunze kuhusu madhara yake na jaribu moja nyumbani kwa majaribio.
• Hakikisha huna mzio (aleji) na Diamox (dawa yenye sulphonamide)
Diamox:Jina asilia acetazolamide(la kibiashara –Diamox)Huweza kutumika kupunguza madhara ya AMS,ni muhimu ambapo ambapo uwanda wa juu hauepukiki.Pia husaidia katika uvutaji pumzi kwa kipindi fulani(Tazama uk.28)Hutumika kuongeza kasi mwili kuzoea kutumia oksijeni kidogo.Lakini hazuii dalili za AMS.Bado unaweza kuathirika kwa maji ubongoni au mapafuni utumiapo.
Watu wengine wana aleji ya Diamox.Kuna madhara yake.Kwa mfano:kusisimka damu kwenye mikono,miguu na uso.Wengine hawaifurahii hali hii ingawa haina madhara na hujitowekea ukiacha kutumia dawa hii.Hukushinikiza kukojoa mno.