Ukimuuliza mtu akutajie safu za milima mirefu kuliko zote duniani,bila shaka atakutajia Himalaya na Andesi.Watu wengi hawajui kwamba milima ya Ulaya ni mirefu hata kuweza kuwasababishia watu magonjwa ya nyanda za juu za milima.Hakika waendao likizo na wanafunzi wa kupanda milima ya Alps aghalabu hawana maarifa ya kutosha au kabisa kuhusu magonjwa ya nyanda za juu.Kuumwa kichwa kwa watalii kutokanako na nyanda za juu kunawezekana,na wengine huugua kwa sababu zingine pia
Kwenye milima ya Alps kuna uwezekano wa kufikia nyanda za juu haraka sana na kirahisi kwa kutumia vigari vya Kamba,njia za reli za milimani na reli-theluji.Njia nyembamba nyingi za milimani huwa na nyanda za juu Zaidi ya mita 2000.
Ziara za kupanda milima ya Alps au sehemu za Ulaya Mashariki huweza pia kukusababishia hatari ya kuugua magonjwa ya nyanda za juu za milima hususan ulalapo katika vibanda vya milimani.
Familia ya watu wane walitumia reli mlima kuanzia Grindelwald(m.1,034)hadi Jungfraujoch,wakatembea hadi kwenye kituo umbali wa m.3650 na kuwa na mandarin.Baada ya muda wa saa 4 katika uwanda wa juu,mvulana wa miaka 11 akalalamika kwa uchungu kuhusu maumivu ya kichwa.Familia ikashuka kwa miguu kisha kwa garimoshi.Mvulana alikuwa mgonjwa wakati wakishuka.Alipofika bondeni alipona haraka.Dalili zake zilidhihirisha magonjwa hatarishi ya maeneo ya milimani(AMS)ambayo familia haikuwahi kusikia.