Swali zuri! Katika hiki kitabu tunazungumzia kuhusu kutoka kwenye mwambao wa bahari kwenda kokote Zaidi ya mita 2000 kutoka usawa wa bahari.Miili yetu huzoea mazingira tuliyomo, tukienda nyanda za juu haina budi kubadilika kulingana na mazingira.
Uwanda wa juu huanza taathira kati ya mita 1500-2000.Mwili huanza kuonekana tofauti kidogo inapojaribu kujihamu dhidi ya mabadiliko ya viwango vya oksijeni.uendapo juu na haraka kwa takribani mita 2500, magonjwa ya nyanda za juu ni kawaida.
Wakipewa muda wa kutosha kubadilika kulingana na mazingira, wengi wanaweza kumudu kusawiri uwanda wa juu wa kati ya mita 5000(Kambi msingi ya mlima Everest) na mita 5500.Zaidi ya m.5500 wachache huweza kumudu kusawiri tena.Afya na uwezo hudhoofika.
Kwa hiyo ni nini tofauti kati ya safari na uwanda wa juu? Tofauti kuu ni kwamba uendapo juu kanieneo hushuka(hewa hupungua) na kwa hiyo kwa kila pumzi utakayovuta kutakuwa na upungufu wa oksijeni kwa ajili ya mwili wako.Oksijeni hutakiwa kwa ajili ya kukupa uwezo wa kutembea,pia huhitajika kukuhuhisha kwa ajili ya ubongo na mmeng’enyo wa chakula kufanya kazi,kukuponya na kazi zote zifanyikazo mwilini mwako bila wewe kujua.
Mwili wako upatapo oksijeni kidogo hujisawiri.Utapumua haraka na kwa mbali sana.Husababisha seli nyekundu za damu kutia oksijeni Zaidi kwenye damu.Mabadiliko huchukua muda ili yatokee. Ukipanda taratibu utabaki na afya njema.Ukipanda haraka utajihatarishia afya kwa kuugua magonjwa ya maeneo ya nyanda za juu kwa mfano magonjwa hatari ya maeneo ya milimani(AMS).