Site Loader

Viungo / Misuli

Watu wengi wanaoabiri wakati wa likizo yenye vitimbwi vingwi huhisi kuumwa au uchungu wa mazoezi ya ya ziada.

Kuwa tayari kabla hujaondoka ni muhimu,kama ni mtelezo barafuni,kutembea,au kuendesha farasi au uendeshaji wa baiskeli ili uifurahie safari yako.

Hakuna utafiti uliofanywa unaonesha kwamba kumwa kwa viungo ni kwa ajili tu kwamba mtu yu kwenye uwanda wa juu.

Viungo vya magoti na misuli ya miguuni ndiyo hasa eneo la tatizo! Bandeji fungishi au vitu vya kufungia huweza kuwa msaada mkubwa.Ni vema kufanya mazoezi ya haja kuimarisha misuli ili kutokuwa na haja ya visaidizi.

Ukitumia fimbo mbili za kutembelea wakati wa matembezi huweza kupunguza uzito kwenye goti hususan kama kuna vijilima vya chini ambapo goti hupata sekeseke nyingi.Hii inaweza kusaidia kama tayari una matatizo ya viungo.

Kupunguza uzito wako (Kama una uzito uliovuka mipaka) au ule wa begi lako.

Kwenye uwanda wa juu:
• Viungo vyako au misuli yako inapoanza kuuma, punguza mwendo. Fikiria siku moja ya kupumzika.
• Kama wewe ni mgonjwa wa maumivu ya viungo, chukua dawa za maumivu uendapo safarini.
• Jotoridi huweza kuwa ya baridi, hakikisha una nguo za joto.

Maandalizi:
• Jiandae na uwe tayari kwa mazoezi yoyote yenye uhalisia na inayoongeza mapigo ya moyo.
• Jaribu uwe na siku nzima ya mazoezi husika kila wiki kwa mwezi kabla ya kuondoka.
• Kama unatumia fimbo za kupandia milima, zizoee kwanza kabla ya kuondoka.

Baada ya kuendesha kwa muda wa saa 6 siku ya kwanza,magoti yangu yalikuwa mauti yangu.Nilijua nilipaswa kuendesha zaidi ya mara tatu kabla ya kuanza safari.Nilikipata kwa siku kadhaa zilizofuata.

Previous         Next